Uhuru ahimiza mataifa yote kukabiliana na uchafuzi wa mazingira

RaisA� Uhuru Kenyatta leo ameyahimiza mataifa yote kuiga mfano wa Kenya katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira kwa kupiga marufuku karatasi za sandarusi. Rais Kenyatta alikuwa akiongea alipofungua rasmi kongamano la tatu la shirika la umoja wa mataifa kuhusu mazingira katika makao makuu ya shirika hilo huko Gigiri, jijini Nairobi. Rais ameyashauri mataifa yote wanachama kutotafuta ufanisi kwa kuharibu mazingira. Rais amekariri mpango wa Kenya wa kupiga hatua zaidi katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira huku akifichua kuwa Kenya ina mpango wa kuongeza ufadhili kwa shirika la UNEP na kuyataka mataifa yote kuiga mfano huo ili kulipa nguvu shirika hilo kutekeleza majukumu yake. Wakati w ahotuba yake , ilibainika kuwa Kenya inapanga kuandaa kongamano la kimataifa kuhusu uchafuzi wa bahari katika robo ya kwanza ya mwaka 2018 kabla ya kongamano la umoja wa mataifa kuhusu bahari duniani litakaloandaliwa mwakaA� 2020 ambalo Kenya inaomba kuwa mwenyeji wake .

Kongamano hilo la UNEA ni kongamano la kiwnago cha juu zaidi linalofanya maamuzi kuhusu mazingira na mwaka huu mkurugenzi mkuu wake Erik Solheim anatumaini kuwa hatua kubwa itapigwa katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira duniani. Kongamano hilo lina mataifa wanachama 193 wa umoja wa mataifa na linahusisha kikamilifu mashirika ya umoja wa mataifa , mashirika maalum , mashirika ya serikali mbali mbali, mashirika ya kijamii na sekta ya kibinafsi. RaisA� Guyana, David Granger,A� amesema mataifa yote yanafaa kukabiliana na uharibifu wa mazingira.