Uhuru adai Raila anachochea wananchi

Rais Uhuru Kenyatta leo amemshtumu kiongozi waA� upinzani Raila Odinga kwa kuwachochea Wakenya kuzusha ghasia. Alisema kiongozi huyo wa upinzani anafuata barabara alioifuata wakati ghasia zilipozuka baada ya uchaguzi mwaka wa 2007. Rais ambaye aliongea huko Sigor katika kaunti ya Bomet, alisema Raila anatumia matamshi yale yale aliyatumia na ambayo huenda yakavuruga umoja miongoni mwa jamii mbali mbali hapa nchini. Rais aliwaambia wakazi wa Sigor kumkatalia mbali gavana Isaac Ruto kwani ameamua kushirikiana na watu wasiozingatia maslahi yao. Jana rais Kenyatta aliwaonya wakazi wa kaunti ya Kericho kujihadhari na njama za upinzani za kuzusha upya ghasia hapa nchini.