Uhuru aagiza Matiang’i kubuni mitihani maalum ya ziada

Rais Uhuru Kenyatta amemwagiza waziri wa elimu Fred Matianga��i kubuni mitihani maalum ya ziada kwa ajili ya kitengo maalum cha wanafunzi wanaoshindwa kufanya mitihani kulingana na ratiba ya kawaida ya mitihani kutokana na sababu mbali mbali. Rais ametoa agizo hilo leo asubuhi alipokutana na Matianga��I afisini mwake katika jumba la Harambee muda mfupi kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darsa la nane mwaka huu. Rais alisema mitihani hiyo maalum itafanywa na wanafunzi ambao huenda walikuwa wagonjwa, walipoteza wazazi wao, au kujifungua wakati wa kawaida wa mitihani. Alisema hivyo ndivyo inavyofanyika tayari katika mataifa mengine duniani huku akikiri kuwa Kenya imesalia nyuma na huu ndio wakati wa kushughulikia hali hiyo.