Uhamishaji wa walimu wakuu waungwa mkono na chama cha kitaifa cha wazazi

Chama cha kitaifa cha wazazi hapa nchini kimeunga mkono uhamishaji unaoendelea wa walimu wakuu wa shule za msingio na sekondari . Mwenyekiti wa chama hicho Nicholas Maiyo amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha uwiano na utangamano wa kitaifa na maadili mema. Amewahimiza walimu wakuu walioathirika kuharakisha kuhama kabla ya muhula mpya . Hatua ya chama hicho kuunga mkono uhamishaji huo imejiri siku chache baada ya chama cha kitaifa cha walimu hapa nchini KNUT kutishia kulemaza shughuli ya ufunguzi wa shule mwezi ujao iwapo tume ya kuwaajiri walimu TSC haitabatilisha uamuzi huo . Katibu mkuu wa chama cha KNUT Wilson Sossion pia amewaagiza walimu wakuu walioathirika kupuuza ilani ya uhamishaji huo iliyotumwa kwao. Walimu wakuu 557 wa shule wameathirika kutokana na uamuzi huo.