Ugonjwa Wa Homa Ya Matumbo Wazuka Zimbabwe

Ugonjwa wa homa ya matumbo umeripotiwa kuzuka katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare A�na kusababisha vifo vya watu wawili. Kuna wasiwasi kuwa huenda maeneo zaidi yakaathirika huku matatizo ya maji na usafi yakizidi kukithiri nchini humo. Maafisa wamesema kuwa kufikia sasa visa A�126 vya ugonjwa huo vimedhibitishwa katika mji mkuu wa taifa hilo A�Harare tangu kuanza kwa msimu wa mvua miezi miwili iliyopita. A�Katika msimu wa mvua wa kati ya mwaka wa 2008/09 ugonjwa huo ulizuka nchini humo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu elfu nne. Ugonjwa wa homa ya matumbo ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria na unaweza kutibiwa. Ugonjwa huo husababisha vifo vya zaidi ya watu elfu A�220 kila mwaka ulimwenguni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya ulimwenguni ya mwaka wa 2014.