Ugonjwa Wa Bacteria Ya Mifugo Waripotiwa Wajir

Kuzuka kwa maradhi ya bacteria ya mifugo kufuja damu kumeripotiwa katika kaunti ya Wajir. Maradhi hayo ambayo yanajulikana kama a�?Qirira�? kwa lugha ya Kisomali na yanaathiri hasa ngamia na mifugo yalizuka katika eneo hilo mwezi Disemba mwaka uliopita wakati mvua ya masika ilipoanza kunyesha na yakaendelea kusambaa hadi mwezi januari na februari mwaka huu. Maradhi hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya mifugo 200 katika sehemu nyingi za kaunti hiyo. Mkurugenzi wa masuala ya mifugo katika kaunti hiyo Dkt. George Kiprono, alisema idara yake imebuni makundi tisa naA� kuyapeleka katika kaunti ndogo sita kuwachanja mifugo dhidi ya ugonjwa huo. Afisa mkuu wa kaunti hiyo anayehusika na kilimo Yussuf Abdi Gedi alisema mifugo wengi wameanza kupata afueni kufuatia matibabu. Sampuli za damu zimepelekwa katika maabara za kituo cha Kabete cha matibabu ya wanyama kufanyiwa uchunguzi.