Uganda Cranes kutumia CECAFA kujinoa kwa mashindano ya bara Afrika

Kocha wa timu ya soka ya Uganda, Moses Basena, amesema watatumia mashindano yajayo baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati; CECAFA kujinoa kwa mashindano ya mwaka ujao ya kuwania kombe la wachezaji wanaosakata soka katika ligi za nyumbani Barani Afrika; yatakayoandaliwa nchini Moroko mapema mwaka ujao.Mashindano hayo yatakayozishirikisha timu 12 kutoka eneo hili A�yataandaliwa humu nchini baadaye mwezi huu. Uganda Cranes itatetea taji yao iliyonyakua mwaka 2015, baada ya makala ya mwaka jana kutoandaliwa kwa kukosa mdhamini. Aidha, CECAFA imethibitisha kuwa magatuzi ya Kakamega, Kisumu na Nakuru A�yataandaaa mashindano hayo huku Machakos na Nairobi pia yakifikiriwa. Mataifa ya Libya na Zimbabwe A�yamealikwa kushiriki katika mashindano hayo kuchukua nafasi za Jibuti na A�Eritrea yaliyoomba kutojumwishwa mwaka huu. Kenya iliandaa mashindano hayo mara ya mwisho mwaka 2013 na kutwaa ubingwa huo baada ya kuishinda timu ya Sudan, mabao mawili kwa bila katika fainali iliyoandaliwa jijini Nairobi.