Uganda Cranes kuchuana na Zanzibari

Mabingwa watetezi Uganda Cranes watachuana na Zanzibari alasiri hii katika mechi ya kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la CECAFA, jijini Kisumu.Uganda itaangazia kunyakua tena taji iliyotwaa mwaka 2015 itakapocheza na Zanzibari katika uwanjani Moi jijini Kisumu. Mshidi wa mechi ya leo atachuana na wenyeji Kenya, waliofuzu kwa fainali baada ya kuishinda Burundi bao moja kwa bila jana. Whyvonne Isuza aliifungia Harambee Stars bao hilo la ushindi dakika ya 95. Kwingineko, aliyekuwa kocha wa AFC Leopards na Gor Mahia, Zdravko Logarusic, ndiye kaimu kocha wa timu ya taifa ya Sudan, huku shirikisho la soka nchini humo likitathmini matokeo yake baada ya mashindano ya Bara Afrika nchini Moroko mapema mwaka ujao. Sudan ilifuzu mashindano hayo kwa mara ya pili kufuatia ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Ethiopia. Aidha, Sudan iliandaa mashindano hayo mwaka 2011. Mashindano hayo, yanayowajumwishwa wachezaji wa ligi za nyumbani yataanza tarehe 12 mwezi Januari hadi nne 4 mwezi Februari. Sudan iko kundini a�?Aa�� pamoja na wenyeji Moroko, Guinea na Mauritania.