Uchunguzi wafanywa kubaini iwapo fedha za kukabiliana na HIV zimeporwa

Wachunguzi kutoka hazina ya kimataifa wako jijini Nairobi kuchunguza iwapo ruzuku yake kwa KenyaA� imeporwa. Hazina hiyo ya Global Fund hasa hufadhili mipango ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya HIV hapa nchini, ugonjwa wa malaria na kifua kikuu. Hazina hiyo hukagua matumizi ya pesa inazotoa kwa mataifa mbali mbali lakini afisa mmoja wa wizara ya afya amesema uchunguzi wa sasa umechochewa na kashfa ya mwaka uliopita ambapo shilingi billion tano zinadaiwa kuporwa kutoka wizara ya afya. Kulingana na wizara ya afya, wakaguzi hao wa matumizi ya pesa waliwasili hapa nchini jumatatu iliyopita na wanatarajiwa kukamilisha uchunguzi wao kesho. Mnamo mwaka 2012, aliyekuwa mkaguzi mkuu wa hazina hiyo John Parsons aliilazimisha Kenya kurejesha shilling million-270 ambazo zilikuwa zimetumiwa vibaya. Marekani imesitisha ruzuku ya takriban shilling bilioni 2.1 kwa wizara ya afya kutokana na madai ya ufisadi na kutowajibika. Mkuu wa shirika la kitaifa la kushughulikia masuala ya watu walio na virusi vya ukimwi nchini Nelson Otwoma amesema mashirika yasiokuwa ya serikali hapa nchini yanahofia kuwaA� wafadhili wengine huenda wakasitishaA� misaada yao kwa Kenya. Kenya itawasilisha ombi kwa hazina hiyo mwezi huu ikitaka kuruhusiwa kutumia shillingi billioni-30 kufadhili mipango ya kukabiliana na virusi vya HIV, ugonjwa wa Malaria A�na kifua kikuu katika kipindi cha mwaka 2018-2020. Hazina ya Global Fund tayari imetenga pesa hizo lakini ili kuzitumia, lazima serikaliitenge kiasi kama hicho kutoka raslimali zake. Hapo jana, waziri wa afya Cleopa Mailu alisema wanasubiri ripoti ya uchunguzikabla ya kuchukua hatua yoyote.