Uchunguzi Wa Virusi Vya Zika Kuimarishwa Mpaka Wa Kenya Na Tanzania

Maafisa wa afya katika mpaka kati ya Kenya na Tanzania wameimarisha uchunguzi kufuatia wasi wasi ulioibuliwa na shirika la afya ulimwenguni kuhusu virusi vya ugonjwa wa Zika. Maafisa hao wamefanya kuwa lazima kwa wasafiri kuchunguzwa kabla ya kuruhusiwa kuvuka mpaka huo. Velid Olando, ambaye ni afisa wa afya katika mpaka huo amesema tangu kutokea kwa virusi hivyo hawajanakili kisa chochote. Olando amesema wana mtambo maalum unaofuatilia kiwango cha joto mwilini na maswala mengine ya aina hiyo na kuwawezesha kubainisha ugonjwa huo. Olando amesema kila wanapobainisha kisa chochote cha kutiliwa shaka wanawafahamisha madaktari mara moja katika hospitatali ya kaunti ya Migori. Wasafiri wengi kwenye mpaka huo hutumia piki piki na kufanya kuwa rahisi kwa raia wa kigeni kuvuka mpaka bila kujulikana.

A�

A�