Uchunguzi kuhusu mchanganyiko wa upasuaji KNH wafichua ukosefu wa utaalam na utepetevu hospitalini humo

 

Uchunguzi wa kamati ya bunge kuhusu mkanganyiko wa upasuaji wa mwezi uliopita katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta umefichua ukosefu wa utaalam na utepetevu katika kuwahudumia wagonjwa katika hospitali hiyo. Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu afya imesikia matukio ya kuogofa ambayo wagonjwa hupitia mikononi mwa wauguzi waliofanya makosa hivi majuzi kwa kumfanyia upasuaji wa ubongo mgonjwa asiyestahili upasuaji huo. Madaktari waliofanya upasuaji huo ambao wote wawili ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi waliwaambia wabunge kuwa walithibitisha maelezo ya mgonjwa huyo kabla ya kumfanyia upasuaji. Madaktari hao walisema walishangaa baada ya kufungua fuvu la mgonjwa huyo na hawangeweza kupata fundo la damu.

Muuguzi aliyekuwa zamuni wakati wa kisa hicho amethibitisha kuwa wagonjwa hao wawili walikuwa wamehamishiwa kutoka kitengo cha kuwalaza wagonjwa hadi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji bila kuwekwa alama zinazohitajika.

Wanachama wa kamati hiyo waliwahoji wauguzi kuhusu jinsi maelezo na alama za john Nderitu aliyehitaji upasuaji wa kichwa zilivyokanganyika na yale yaA� Samuel Kimani ambaye hakuhitaji upasuaji huo.