Uchumi Wa Nchi Umeimarika,Asema Waziri Wa Fedha

Waziri wa fedha Henry Rotich amesema uchumi wa nchi hii unaindelea kuimarika licha ya changamoto nyingi ikilinganishwa na chumi za nchi zingine.Akisema kwamba uchumi wan chi hii unaendelea kukua kwa asilimia 5.6 Rotich alisema uchumi wan chi hii umeripotiwa kuwa miongoni mwa chumi zinazokua kwa haraka duniani.Akiwasilisha bajeti ya kipindi cha matumizi ya pesa za serikali cha mwaka 2016/2017 katika majengo ya bunge,Rotich alisema ili kuafikia matarajio ya wakenya, ipo haja ya kuzingatia zaidi suluhu za muda mrefu.Alisema ipo haja ya kupunguza gharama ya kufanya biashara na kuwekeza zaidi katika usalama na kilimo ili kupunguza umasikini.

Rotich alisisitiza haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa karibu wa kikazi na serikali za kaunty ili kufanikisha magatuzi, kuimarisha afya na kuyasaidia makundi yanayokabiliwa na changamoto nyingi.