Uchumi Wa Ghana

mahama

Rais John Mahama wa Ghana amewahakikishia wafuasi wa chama chake kuwa serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambayo itarejesha taifa hilo kwenye mkondo wa ufanisi.

Alitoa hakikisho hilo jana alipozindua kampeni za uchaguzi wa urais unaotarajiwa kuwa kinyang’any’iro kikali zaidi nchini humo. Matatizo ya kiuchumi yameathiri utawala wa rais Mahama ambaye anawania hatamu nyingine ya urais. Mahama atakabiliana na mpinzani wake, Nana Akufo-Addo ambaye ni kiongozi wa chama cha New Patriotic.

Ghana ilikuwa mojawapo wa nchi zilizo na kiwango cha juu cha ustawi wa uchumi barani Afrika kutokana na biashara ya dhahabu, kakao na mafuta. Hata hivyo ukuaji huo umedorora tangu mwaka-2014 kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa, hatua iliyosababisha msukosuko wa kifedha na kutekelezwa kwa hatua za ufufuzi wa uchumi.