Uchaguzi Wafanyika Kwenye Wadi Nne Nchini

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kwa wakati huu inaendesha uchaguzi katika wadi nne katika kaunti nne za Kajiado, Kisii, Tana River na Turkana. Zoezi hilo lilianza mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi kama lilivyopangwa. Hata hivyo taarifa zasema kuwa kulikuwa na hali ya wasi wasi katika sehemu za wadi ya Kalokol huko Turkana ambako milio ya risasi ilisikika jana usiku huku watu wawili wakidaiwa kupata majeraha katika hali zisizoeleweka. Taarifa zimesema kwamba milio ya risasi ilisikika hewani wakati wa usiku huku wafuasi wa vyama pinzani vya Jubilee na ODM wakionyesha umaarufu wao. Kutokana na hayo msichana mdogo wa umri wa miaka minne alipata majeraha ya risasi. Hali ya wasi wasi iliendelea katika vitio vya kupigia kura vya Lochuga baada ya wafuasi wa wagombea wawili ambao ni Josphat Ekenu wa ODM na Simon Nanga��iro wa Jubilee walizozana na kutatiza utaratibu wa upigaji kura. Hata hivyo upigaji kura uliendelea baada ya maafisa wa usalama kuingilia kati na kuyafukuza makundi hayo mawili. Zaidi ya wapiga kura elfu 20 waliosajiliwa wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo mdogo katika wadi hizo nne za Mosiro katika kaunti yaA�A�Kajiado, Sala katika eneo bunge laA�A�Bura kaunti ya Tana River, NyachekiA�A�katika eneo bunge la Bobasi kaunti ya Kisii na Kalokol katika eneo bunge la TurkanaA�A�ya kati kaunti ya Turkana. Maafisa 320 wa IEBC wanasimamia zoezi hilo katika vituo 64 vya kupigia kura.