Uchaguzi Wa Kumtafuta Kiongozi Wa FIFA Wafanyika

Uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Sepp Blatter kama kiongozi wa soka duniani FIFA unatarajiwa kufanyika leo. Uchaguzi huo utakaofanyika mjini Zurich unatarajiwa kufanywa na wajumbe 207.Blatter, 79 Alinga��atuka mwaka jana kutokana na tuhuma za ufisadi zilizogubika shirikisho hilo.Kuna wagombea watano wanaotaka kumrithi ambao ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne.Ili kutangazwa mshindiA� mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa.Fifa imesema lazima mshindi ajulikane leo Ijumaa.