Uhuru arai wakenya kuombea taifa

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa uchaguzi mpya wa urais utaandaliwa tarehe-26 mwezi huu jinsi ilivyoratibiwa. Rais Kenyatta amewahimiza wakenya kuungana kwa maombi ya kitaifa Jumapili ijayo kuombea umoja wa taifa hili na kuwatahadharisha wananchi na viongozi wa kisiasa kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga taifa hili. Akiongea katika ikulu ya Nairobi, rais Kenyatta aliwahimiza viongozi kuthamini maisha ya Wakenya kuliko maslahi yao ya kibinafsi.

Rais alitoa hakikisho hilo baada ya kujiuzulu kwa Roselyn Akombe kutoka tume ya IEBC akitaja sababu kadhaa ikiwemo kuingiliwa kwa tume hiyo na wanasiasa.