Uchaguzi Kuendelea Nchi Ya Niger

Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea katika nchi ya Niger baada ya kukamilika kwa upigaji kura za urais na ubunge jana.Rais Mahamadou Issoufu anatarajiaA� kushinda kipidi cha pili katika taifa hilo fukara laA� Afrika magharibi.Mpinzani wake mkuu Hama Amadou kwa sasa yuko korokoroniA� kwa kosa la ulanguzi wa watoto,dai ambalo amekanusha.Shughuli ya upigaji kura ilifanywa chini ya ulinzi mkali,huku ikicheleweshwa katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo, Niamey.Kulikuwa na hofuA� kwamba wanamgambo wa kiislamu katika nchi jirani za Nigeria,Mali na LibyaA� kutekeleza visa vya uhalifu.Kulitokea visa vya ghasia kabla yaA� shughuli hiyo ya upigaji kura ,hasa unyanyasajiA� na mzozo kuhusu karatasi za kupigia kura.Serikali ya nchi hiyo imesema kuwa takriban raia milioni 1.5A� hawana vitambulisho vya kitaifa,lakini wataruhusiwa kupiga kura baada ya kuthibitishwa,jambo ambalo limepingwa vikali na upinzani.Taifa la Niger lina utajiri mkubwa wa maliasili,yakiwemo madini ya uranium na mafuta,lakini ni miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani kulingana naA� umoja wa mataifa.