Uchaguzi Congo kufanyika 2018

Maafisa wa uchaguzi kwenye Jamhuri ya ki-Demokrasia ya Congo wamesema uchaguzi wa Urais uliocheleweshwa kwa muda mrefu, A�hatimaye utafanyika mwezi desemba mwaka 2018. Hivi majuzi tume ya uchaguzi nchini A�humo ilikuwa imesema uchaguzi hauwezi kufanyika hadi angalau mwaka 2019, ikitaja ghasia zinazoendelea katika eneo la Kasai na pia changamoto nyinginezo. taifa hilo limeshuhudia ghadhabu ya raia wake kuhusiana na hatua ya Rais joseph kabila kukataa kuacha madaraka hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika desemba mwaka 2016. Kabila aliingia madarakani baada ya kuuawa kwa Babake mwaka 2001, na aliweza kuchagulwia tena mwaka 2006 na pia mwaka 2011.