UASU yatishia kufanya maandamano

Chama cha wahadhiri wa vyuo vikuu UASU, kimesema kitafanya maandamano makubwa katika vyuo vyote vikuu vya umma kote nchini siku ya Jumatano.Chama hicho kimesema kuwa baada ya majadiliano kimeamua, kuzindua upya mgomo wake kufuatia hatua ya serikali ya kusita kushughulikia matakwa yao.Mwezi jana serikali ilitangaza nyongeza ya shilingi bilioni kumi kwa mishahara ya wahadhiri,ambayo walipuzilia mbali, isipokuwa vyama vya KUDHEHIA na KUSU, ambavyo vilitia saini makubaliano hayo.Akiongea na shirika la utangazaji la KBC, mwenyekiti wa kitaifa wa jopo la mahojiano la UASU Prof Joseph Mberia alisema wamewasilisha pendekezo lao la tatu na la mwisho kwa baraza la pamoja la ushauri la vyuo vikuu vya umma na sasa wanasubiri baraza hilo kuwasilisha mapendekezo yake.Wakati huo huo,mwenyekiti wa kamati ya majadiliano ya baraza hilo la pamoja la PPUCF Issac Mbechi ametoa wito kwa wahadhiri kukubali nyongeza hiyo ya bilioni kumi. Prof Mbechi alisema wahadhiri hao wanaweza kujadili masharti bora kati ya miaka ya 2017 na 2021 akisema matakwa yao kwa sasa hayawezi kutekelezwa