UASU yaofia kuchelewa kwa serikali kuwasilisha pendekezo lake

Chama cha wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma sasa kina wasi wasi kuhusu kuchelewa kwa serikali kuwasilisha pendekezo lake kuhusiana na mgomo unaoendelea kuhusu makubaliano ya pamoja ya mwaka 2013. Mwenyekiti wa chama cha wahadhiri wa vyuo vikuu (UASU) George Bosire sasa analaumu mkutano wa ushauri wa baraza la vyuo vikuu vya umma kwa kushindwa kutoa pendekezo la utekelezaji wa makubaliano hayo ya pamoja. Katibu mkuu wa chama hicho Dr. George Omondi ameihimiza serikali kutatua mzozo huo ili kuokoa elimu ya juu ya nchi hii isisambaratike. Pia wahadhiri wa vyuo vikuu wameelezea wasi wasi kuhusu kuitokea kwa taarifa kadhaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa mgomo wao umemalizika.