Wahadhiri wa vyuo vikuu wasitisha mgomo

Wahadhiri wa chuo kikuu wamesitisha mgomo wao wa siku 54 baada ya chama cha wahadhiri wa vyuo vikuuA� UASU kutangaza kuwa hatimaye kimetia saini mkataba wa pamoja na serikali. Mkataba huo unaowianisha mishahara katika vyuo vyote vikuu utawawezesha wahadhiri hao kupata nyongeza ya mshahara ya asilimia 17.5 pamoja na ongezeko la marupurupu ya nyumba kwa asilimia 3.9 . Chama hicho pamoja na baraza la mashauriano la vyuo vikuu vya umma zimewaagiza wahadhiri wote kurejea kazini hapo kesho.Katibu mkuu wa UASU Constantine Wasonga, alisema uamuzi huo ulikuwa wa pamoja na uliafikiwa baada ya mashauriano na kina. Alisema kati ya shilingi bilioni 10, chama cha UASU kitapokea kitita cha shilingi bilioni sita wakati mmoja. Mkataba huo wa pamoja utaanza kutekelezwa kuanziaA� mwezi Julai mwaka 2013 katika vyuo vyote vikuu isipokuwa chuo kikuu cha Masaai Mara ambacho hakikuwa sehemu ya mkataba huo. Mkataba wa kurejea kazini uliotiwa saini na chama hicho na baraza hilo, unasema kuwa wahadhiri na maafisa wa chama hicho walioshiriki katika mgomo huo , hawatachukuliwa hatua zozote za kinidhamu .

A�