Uamuzi wa kina kuhusu uchaguzi wa tarehe 8 Agosti kutolewa wiki hii

Mahakama ya juu wiki hii inatarajiwa kutoa uamuzi kamili baada ya kutangua uchaguzi wa urais tarehe 8 mwezi Agosti. Jaji mkuu David maraga, naibu wake Philomena mwilu, majaji Smokin Wanjala na Isack Lenaola ambao walitoa uamuzi huo kwa wingi wa kura nne dhidi ya majaji wawili ambao hawa-kukubaliana na uamuzi huo wamekuwa wakiandika uamuzi huo. Majaji hao wanapanga kukutana kuwianisha uamuzi wao. Haya yanajiri huku rufani ikiwasilishwa na mbunge wa Nyeri mjini Ngunjiri Wambugu kuhusu madai ya utovu wa maadili wa Jaji Mkuu. Baadaye aliondoa rufani hiyo kutokana na shinikizo la umma.