Tusker na AFC Leopards kuchuana alasiri hii

Timu za Tusker na AFC Leopards zinazoshiriki katika ligi ya Sportpesa humu nchini, zitajitosa ugani alasiri hii hukuA� mechi za kuwania kombe la a�?Sportpesa Supera�? zikinga��oa nanga katika uwanja wa Uhuru jijini Dar-es-Salaam, Tanzania. AFC Leopards itacheza mechi ya ufunguzi katika michuano ya mchujo ya timu nane dhidi ya Singida United ya Tanzania chini ya ukufunzi wa kocha mpya Dorian Marian kutoka Romania huku mabingwa watetezi wa ligi ya Sportpesa humu nchini Tusker wakimenyana na miamba wa soka nchini Tanzania Yanga. Kombe hili linajumwisha timu nne za humu nchini; Gor Mahia, AFC Leopards, Tusker na Nakuru All Stars na nne za Tanzania; Yanga, Simba, Singida United na Janga��ombe. Timu itakayonyakua taji hiyo itatia kibindondi shilingi milioni tatu,nambari mbili itatuzwa shilingi milioni moja. Aidha, timu zitakazobanduliwa katika nusu fainali zitapokea shilingi nusu milioni na zitakazobandiliwa katika robo fainalini zitatuzwa shilingi laki mbili unusu. Wakati uo huo, timu itakayotwaa ushindiA� itapata fursa ya kumenyana na timu ya Everton inayoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza. Everton itatumia mchuano huo kujiandaa kwa msimu ujao wa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.