Tume Ya Utangamano Yahimiza Amani Katika Eneo La North Rift

Tume ya utangamano na mshikamano wa kitaifa imezindua mikutano kadhaa ya majadiliano katika eneo la North Rift katika juhudi za kudumisha amani na maendeleo katika eneo hilo. Tume hiyo inajumuisha viongozi waliochaguliwa pamoja na wale wa kidini kwenye majadiliano hayo ya kuleta amani hasa katika maeneo yanayozongwa na ghasia na visa vya wizi wa mifugo huko Elgeyo-Marakwet A�na A�Pokot Mashariki. Mwenyekiti wa tume hiyo ya NCIC,A�Francis Ole Kaparo amesema mashauriano hayo yatakayoendelea kwa majuma kadhaa yanalenga kuwajumuisha viongozi katika harakati za muda mrefu za kudumisha amani. Akiongea kwenye mkutano huko Nakuru, Kaparo aliwataka viongozi kuandaa mikutano ya pamoja ya amani katika maeneo hayo ili kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika juhudi hizo za kuleta amani kwa ajili ya mshikamano wa kijamii.