Tume Ya Ugavi Mapato Kushinikiza Serikali Ya Taifa Kuongeza Mgao Wa Pesa

Micah-Cheserem-CRA-Chairman
Mwenyekiti wa tume ya ugavi mapato Micah Cheserem amesema tume hiyo itaishinikiza serikali ya taifa kuongeza mgao wa pesa kwenye kaunti ili kufadhili miradi zaidi ya maendeleo. Cheserem alisema hata ingawa mfumo wa ugatuzi umeleta maendeleo kwenye kaunti, ipo haja ya kuongeza pesa zinazotengewa kaunti na kutolewa kwa pesa hizo kwa wakati unaofaa ili kuhakikisha serikali hizo zitatekeleza miradi ya maendeleo ipasavyo.
Akiongea alipotembelea hospitali ya Kakamega, Cheserem alisema tume hiyo itashirikiana na afisi ya mhasibu mkuu wa serikali na tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi ili kuhakikisha wanachama wa mabunge ya kaunti ambao wamepora mali ya umma kupitia kwa ziara zisizo na msingi wamechukuliwa hatua.

Alitoa wito kwa idara ya mahakama kuharakisha kesi za ufisadi hapa nchini ili kuhakikisha wanaotekeleza ufisadi wamechukuliwa hatua za kisheria. Aidha alitoa wito kwa wananchi na vyombo vya habari kutosita kutoa habari kuhusu ufisadi