Tume Ya Uganda Kuomba Msamaha Dhidi Ya Uchaguzi

Tume ya uchaguzi ya Uganda imeomba msamaha kutokana na hatua ya kuchelewa kufungua vituo vya kupiga kura huku watu wakipiga foleni kushiriki katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Tume hiyo ilisema hatua hiyo ilitokana na matatizo katika usafirishaji vifaa vya kupiga kura. Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni anawania kipindi cha tano cha uongozi baada ya kuwa mamlakani kwa miaka-30 huku wagombeaji-7 wakiwania urais katika kinyang’anyiro hicho kilichovutia mashindano makali zaidi.