Tume ya IEBC Yazindua Shughli Ya Usajilishaji Wapiga Kura

Awamu ya kwanza ya shughuli ya kuwasajili wapiga kura wapya ilizinduliwa jana huku mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Issaak Hassan akitoa wito kwa wakenya kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa.Akiongea wakati wa uzinduzi wa shughuli hiyo katika ukumbi wa kijamii wa Pumwani ,Isaac Hassan alisema kuwa awamu hiyo ya kwanza inalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni nne.Mwenyekiti huyo alidokeza kuwa tume hiyo imenunua mitambo elf 5,756 ya kuwasajili wapiga kura .