Tume Ya EACC Yafichua Jinsi Pesa Za Kugharamia Elimu Katika Shule Zilivyoporwa

Tume ya kukabiliana na ufisadi nchini imetoa ripoti inayofichua jinsi mamilioni ya pesa za kugharamia elimu bila malipo katika shule za msingi zilivyoporwa. Akipokea ripoti hiyo iliyotayarishwa kutoka shule 42 katika kaunty kumi na moja, waziri wa elimu Dr Fred Matianga��i alimuagiza mwenyekiti wa chama cha walimu wakuu wa shule za msingi za umma nchini Shem Ndolo kuhakikisha waliohusika na uporaji wa pesa hizo wameshtakiwa.
Ripoti hiyo inaonyesha jinsi walimu wakuu wa shule wamekuwa wakitumia pesa hizo kujinufaisha huku wengi wao wakijipatia mikopo isiyokuwa na wadhamini, kukiuka sheria za ununuzi wa vitabu,kujilipa marupurupu bandia ya usafiri nga��ambo na vile vile marupurupu ya kuhudhuria mikutano. Akikabidhi ripoti hiyo, mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Halakhe Waqo aliwashutumu wakuu hao wa shule kwa kuubadilisha mpango wa elimu bila malipo katika shule za msingi kuwa wa kujitajirisha na akaihimiza serikali iwashtaki waliohusika na wizi huo.
Mapema mwaka huu waziri Matiangi aliagiza uchuguzi ufanywe baada ya kuzuru shule kadhaa na kupata zikiwa katika hali duni.Ripoti hiyo inapendekeza wizara ya elimu ichukue hatua za kuziba mianya ya uporaji wa pesa hizo.