TSC yapuuzilia mbali malumbano kati yake na KNUT

Tume ya kuajiri waalimu nchini TSC imepuuzilia mbali malumbano ya hivi majuzi kati yake na chama cha kitaifa cha waalimu (KNUT), ambayo yalishuhudia pande hizo mbili kuahirisha mazungumzo  yaliyolenga kuondoa maswala tata.

Mwenyekiti wa (TSC), Dr. Lydia Nzomo anasema tume hiyo bado imejitolea kuboresha matokeo ya mitihani ya kitaifa na pia maslahi ya waalimu, akiongeza kwamba tume hiyo bado iko wazi kwa mazungumzo na chama hicho cha waalimu katika juhudi za kuafiki suluhu juu ya malalamishi ya waalimu.

Mkutano wa faragha wa siku tano kati ya TSC na (TSC) wiki hii umefutiliwa mbali, kufuatia hali ya kuto-elewana kuhusu matakwa ya (KNUT) ya kubatilisha uhamisho wa waalimu wakuu 85. Ilani ya kufanya mgomo iliyotolewa na chama hicho cha (KNUT), imejiri mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa mtihani wa kitaifa  wa darasa la nane (KCPE), na ule wa kidato cha Nne (KCSE).