TSC laitikia shinikizo na kutoa barua za uhamisho kwa waalimu wasio wenyeji katika eneo zao

Tume ya kuwaajiri waalimu-TSC imeitikia shinikizo na kutoa barua za uhamisho kwa waalimu wasio wenyeji na nafasi zao kujazwa na waalimu ambao ni wenyeji katika eneo la kaskazini-mashariki mwa nchi. Waalimu wasio wenyeji kutoka kaskazini mashariki mwa nchi walikuwa wamepiga kambi katika makao makuu ya tume ya kuwaajiri waalimu jijini Nairobi wakitaka uhamisho kufuatia mauaji ya hivi majuzi ya waalimu wawili huko Wajir. Waalimu hao walikuwa wameapa kuto-rejea katika eneo hilo wakisema usalama wao haujahakikishiwa licha ya serikali kutoa hakikisho. Hatua hiyo ya tume ya TSC hata hivyo imewakera baadhi ya viongozi wa eneo hilo huku kiongozi wa walio wengi katika bunge la taifa Aden Duale akidai hatua hiyo itazorotesha ubora wa elimu katika eneo hilo.