Trump Kuwafunga Jela Wahamiaji Haramu Marekani

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema kuwa atawarejesha makwao au kuwafunga jela wahamiaji haramu wapatao milioni tatu wanaoishi nchini Marekani. Trump alisema kuwa wale wanaolengwa watakuwa wahamiaji walio na rekodi za uhalifu na wanaojihusisha na magenge ya dawa za kulevya. Trump alisema kuwa anapanga A�kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico na kueka ua katika eneo hilo. Inakisiwa kuwa kulikuwa na wahamiaji haramu wapatao elfu 178 walio na rekodi za uhalifu nchini Marekani mwaka wa 2010 kwa mujibu wa ripoti moja ya Congress. Inasemekana kuwa kuna wahamiaji wapatao milioni 11 ambao hawana stakabadhi maalum nchini Marekani wengi wao wakisemekana kutoka A�Mexico. Trump anatarajiwa kuapishwa rasmi tarehe 20 mwezi Januari mwakani ili kuchukuwa mahala pa Barack Obama ambaye ameliongoza taifa hilo kwa mihula miwili iliyopita.