Trump kutia saini agizo jipya la kirais kuhusu uhamiaji

Rais  Donald Trump anatarajiwa kutia saini agizo jipya la kirais  kuhusu uhamiaji hivi leo baada ya rufaa za mahakama kuzuia agizo lake la hapo awali. Duru  zinaarifu kuwa Iraq huenda ikaondolewa katika orodha hiyo ya mataifa saba ya kiislamu yaliyoathiriwa na marufuku hiyo ya muda  ya uhamiaji na kutoa makazi mapya kwa wakimbizi. Aliyekuwa waziri wa maswala ya usalama wa ndani  Michael Chertoff amesema kuwa anatumai kuwa rais  huyo atatoa agizo ambalo linakubalika bila kumbagua yeyote. Agizo la awali lililotiwa saini na Trump tarehe 27 mwezi Januari lilijumuisha mataifa ya  Iraq,  Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen.