Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel

Rais Donald Trump wa Amerika atatambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa A�Israel,kulingana na maafisa wakuu wa serikali yake.Trump anatarajiwa kutangaza hayo kwenye hotuba baadaye hii leo.Kiongozi huyo pia anatarajiwa kuagiza kuhamishwa kwa ubalozi wa Amerika kutoka mji wa A�Tel Aviv hadi Jerusalem, lakini agizo hilo litatekelezwa baada ya kipindi cha miaka kadha.Israel imeunga mkono hatua hiyo lakini viongozi wa kiarabu na wale wa Kipalestina wameonya kwamba hatua hiyo itaathiri pakubwa juhudi zozote za kuleta amani huko mashariki ya kati.Saudi Arabia,ambayo ni mshirika wa karibu wa Amerika imekashifu vikali hatua hiyo. Israel imekuwa ikidai mji wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu huku nao wapalestina wakidai mji wao mkuu wa Jerusalem mashariki.Katika kutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel,Amerika ndio taifa la kwanza kufanya hivyo tangu kubiniwa kwa taifa hilo la kiyahudi mwaka 1948.Mji wa Jerusalem ni makao ya dini mbali mbali.