Trump awarai Ma-Senete kuunga mkono mushwada wa bima ya afya

Rais Donald Trump wa Marekani amewarai ma-seneta wa chama cha  Republican kuunga mkono muswada wa sheria ya chama chake kuhusu bima ya afya, mnamo siku ya mkesha wa kuupigia kura muswada huo. Bunge la Seneti la Marekani litapiga kura hivi leo, huku wajumbe wa chama cha  Republican wakijaribu kufanikisha  juhudi zao za kufanyia marekebisho  sheria hiyo ya Rais wa zamani  Barack Obama.  Lakini miongoni mwa Ma-seneta hao wa chama cha Republican kuna wasiofahamu juu ya muswada huo, na pia haijulikani iwapo utapitishwa.