Trump atazama tukio la jua kupita nyuma ya mwezi

Raia nchini Marekani akiwemo rais Dolnad Trump, jana walitazama juu huku jua likipita nyuma ya mwezi kwenye tukio ambalo lilishuhudiwa kote nchini humo kwa mara ya kwanza katika muda wa karne moja. Mamilioni ya watu nchini Marekani walikusanyika kwenye vikundi kushuhudia tukio hilo ambapo mwezi ulizuia mwangaza wa jua kwa muda mfupi. Hafla za aina mbali mbali ziliandaliwa nchini humo kwa kile kilichotajwa kuwa tukio lililopigwa picha na watu wengi zaidi katika siku za hivi punde. Katika mji mkuu wa Washington, raisA�A� Donald Trump alitazama tukio hilo kutoka ikulu ya White House akiwa na mkewe Melania na mwanawe Barron.