Trump atangaza rasmi kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa Israel

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza rasmi kuwa taifa hilo sasa linautambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa taifa la Israel na hivyo kukiuka sera rasmi ya miongo kadhaa ya taifa hilo.Trump ameelezea hatua hiyo kuwa iliochelewa kutekelezwa.Hatima ya mji huo muhimu wa kale ni miongoni mwa maswala nyeti yanayochachusha uhusiano baina ya taifa la Israel na wapalastina.Trump ametaja hatua hiyo kuwa ya kihistoria,licha ya shutuma kali za kimataifa.Kutokana na hatua hiyo, rais wa wapalastina Mahmoud Abbas ametaja uamuzi huo kuwa wa kusikitisha,huku akisema Marekani kamwe haitasalia kuwa mpatanishi huko mashariki ya kati.Mataifa manane,miongoni mwa mataifa 15 ambayo ni wanachama wa Umoja wa mataifa yametaka mkutano wa dharura kuandaliwa kufikia mwishoni mwa juma hili ili kujadili uamuzi huo wa Marekani.