Trump ashinda Mississipi na Michigan

Donald Trump-mgombea anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani-amejiongezea ushawishi kama mgombea mkuu kufuatia ushindi wake katika majimbo ya Michigan na Mississippi.

Trump alisema kuwa anakiongezea umaarufu chama cha Republican. Mshindani wake mkuu Seneta Ted Cruz naye alipata ushindi katika jimbo dogo la Idaho.

Upande wa chama cha Democrats Bernie Sanders ameshinda mchujo katika jimbo la Michigan huku naye Hillary Clinton akiibuka mshindi katika jimbo la Mississipi.