Trump Ashambuliwa Katika Mjadala Wa Republican

Mwaniaji urais wa chama cha Republican nchini marekani Donald Trump ameshtumiwa na wapinzani wake kwenye mjadala wa chama hicho baada ya siku ambapo wanasiasa wakongwe wa chama hicho waliwahimiza wapigaji kura kutomchagua. Kwenye mjadala huo, Trump alisema kwamba amebadili msimamo wake wake kuhusiana na maswala kadhaa. Wanachama wakuu wa chama cha Republican walisema kuwa Trump atashindwa kwenye uchaguzi huo wa urais.