Trump asema marekani haitavumilia hujuma za kibiashara

Rais Donald Trump wa Marekani amesema nchi hiyo haitavumilia tena hujuma za kibiashara kutoka kwa nchi wanachama wa jumuia ya Asia na Pacifiki. Akihutubia kongamano la viongozi kutoka jumuia hiyo nchini Vietnam Rais Trump alisema Marekani iko tayari kushirikiana na nchi za shirika la APEC, mradi tu zikomeshe hujumua za kibiashara. Trump amesema Marekani haitakubali kutumiwa na nchi hizo kwa manufaa yao ya kibiashara. Tayari Marekani imeapa kuchukua hatua za kuziba nakisi ya kibiashara kati yake na China na Japan. Alipochukua hatamu za uongozi, rais Trump alitishia kuindoa Marekani kwenye mkataba huo wa kibiashara unaojumuisha nchi 21 za eneo la Asia na Pacific akisema mkataba huo hauna manufaa kwa uchumi wa Marekani.A� Kwa jumla uchumi wa nchi hizo-21 unachangia asilimia-60 ya pato lote la kifedha duniani.