Trump asambaratisha mpango wa kutoa matibabu wa Obama Care

Rais A�Donald Trump wa Marekani ametangaza kusambaratika kwa mpango wa kutoa matibabu ulioanzishwa na aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama baada ya mswada wa matibabu wa chama cha A�Republican kupitishwa A�kwa kura chache katika bunge la chini la A�Congress. A�Mswada huo ulipitishwa kwa kura 217 kwa kura 213. Wanachama wa Democrats A�wamesema kuwa mswada huo mpya utawaacha mamilioni ya raia bila bima ya matibabu. Mswada huo sasa utapelekwa A�katika bunge la A�Senate ambapo wanachama wa Republican waliashiria kuwa watauweka kando na kuratibu sheria mpya. Waandamanaji waliandamana kupinga sheria hiyo mpya.