Trump amsifu Xi Jinping alivyoshughulikia tisho la Korea Kaskazini

Rais wa Marekani, Donald Trump amemsifia mwenzake wa Uchina Xi Jinping kuhusu jinsi alivyoshughulikia tisho laA� kutoka Korea Kaskazini. Trump aliwashangaza wengi pale aliposema halaumu serikali ya Uchina kwa kuchukua fursa zinazojitokeza nchini Marekani kuhusiana na biashara kati ya mataifa hayo. Trump yuko ziarani nchini Uchina kama sehemu ya ziara yake ya mataifa matano barani Asia. Awali, Trump alihimiza Korea Kaskazini kushitisha mipango yake ya kiniuklia huku akitahadharisha taifa hili dhidi ya kutoa vitishio kwa Marekani na mataifa mengine.