Trump Ajipatia Tiketi Ya Kuwakilisha Chama Cha Republican

Donald Trump amejipatia tiketi ya kuwakilisha chama cha Republican katika uchaguzi mkuu ujao wa urais nchini Marekani mwezi Novemba mwaka huu. Hii ni baada ya miezi kadhaa ya kampeini zake tata zilizoigawanya Marekani kisiasa. Juhudi za wale wanaompinga mfanyibiashara huyo mkwasi za kuwashawishi wajumbe kutomteua Trumph hazikufua dafu. Raia wengi wa Marekani hawajakuwa wakifurahia matamshi na msimamo mkali wa Trumph. Aidha amekuwa akiitisha kupigwa maarufuku kwa waislamu kuingia nchini Marekani.