Trump Afanya Uteuzi Muhimu

Rais mteule wa Amerika Donald Trump amemteua mtaalam wa kiuchumi Peter Navarro kuwa mkuu wa baraza la kibiashara nchini humo. Navarro ataliongoza baraza hilo na kuhudumu kama mkurugenzi wa sera za biashara na viwanda.

Navarro alikuwa mshauri wa Trump wakati wa kampeini za uchaguzi. Miongoni mwa vitabu alivyo chapisha ni vile vya The Coming China Wars na Death by China ambavyo vinashtumu vikali sera za China. Wakati wa kampeini zake, Trump alikashufu vikali makubaliano ya kibiashara yaliofikia baina ya Amerika na mataifa kama vile China na Mexico.Tayari Trump ameikashfu hadharani China.