Trump Aendelea Kuongoza Katika Chama Cha Republican

Mashindano makali ya kinyang’anyiro cha kupata idhini ya vyama kuwania urais yanaendelea katika jimbo la Massachusetts na Alaska nchini Marekani. Donald Trump anaongoza katika chama cha Republican naye Hillary Clinton anaongoza katika chama cha Democratic baada yaA�kura ya mchujo katika majimbo manne kuhesabiwa. Seneta Ted Cruz anajitahidi ili asishindwe na Trump huko Texas, jimbo alikozaliwa. Clinton anatumai kuimarisha ushindi wake wa miwhsoni mwa wiki katika jimbo la South Carolina, ambako alipata kura nyingi miongoni mwa Wamarekani wa asili ya kiafrika na kudumisha umaarufu wake wa kisiasa baada ya kushindwa katika jimbo la New Hampshire na Bernie Sanders. Hapo Novemba 8 mwaka huu Amerika itamchagua Rais atakayechukua mahala pa Rais Barack Obama, ambaye ni wa chama cha Democratic baada ya kukamilisha vipindi viwili ofisini ambavyo chama cha Republican kilichukua udhibiti wa mabunge yote mawili ya Congress.