Tottenham Hotspurs Yailemea Southampton

Dele Alli alitia kimiani mabao mawili huku Tottenham Hotspurs ikiendelea kufufua matumaini ya kushiriki kwenye ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya baada ya kuilaza Southampton mabao manne kwa moja katika mechi ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza iliyochezwa jana usiku uwanjani St Marys. Southampton ilifunga kwanza katika dakika ya pili kupitia Virgil van Dijik aliyepokea krosi murwa kutoka kwa James Ward. Hata hivyo, Spurs ilisawazisha kabla ya mapumziko kupitia Delle Ali. Dakika chache baada ya mapumziko, Harry Kane aliifungia Tottenham bao la pili baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Christian Eriksen kisha Son Heung-Min na Alli wakaifungia Spurs mabao mengine mawili. Spurs sasa imesalia katika nafasi ya tano ligini, alama moja nyuma ya Asenali.