Tobiko atangaza Dorcas Oduor kuchukua nafasi yake

Aliyekuwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko ametangaza kwamba katibu wa mashtaka ya umma Dorcas Oduor atasimamia afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma kabla yaA�A�mkurugenzi mwingine wa mashtaka ya umma kuteuliwa. Akiwahutubia maafisa wakuu wa Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kutoka makao makuu na kaunti zote 47 ambako kuna afisi za idara hiyo, mkurugenzi wa mashtaka ya umma anayeondoka alisema kuondoka kwake hakujaacha pengo lolote katika iliyokuwa afisi yake akisema amewaacha maafisa walio na ujuzi wa hali ya juu na afisi hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida. Alisema ana imani katika utenda kazi wa maafisa alioacha nyuma huku akisema afisi hiyo iliimarisha huduma alipokuwa mamlakani. Rais Uhuru Kenyatta wiki iliyopita aliwateua Keriako Tobiko, aliyekuwa seneta wa Turkana John Munyes na aliyekuwa gavana wa Marsabit Ukur YattaniA�A�kuwa mawaziri.