Tobiko akana kuidhinisha mashtaka dhidi ya dereva wa Wahome

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma A�Keriako Tobiko amefafanua kuwa hajaidhinisha mashtaka yoyote dhidi ya dereva wa aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nyeri marehemu Wahome Gakuru jinsi ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari . Hata hivyo Tobiko amesema ameagiza faili yake kutoka kwa polisi ili kudurusu na kutoa maagizo. Haya yanajiri baada ya kuripotiwa kuwa dereva wa marehemu Gakuru , Samuel Kinyanjui, alitarajiwa kufikishwa katika mahakama ya A�Kigumo kujibu mashtaka ya uendeshaji kiholela wa gari uliosababisha kifo cha Gakuru. Gakuru alifariki wiki iliyopita kufuatia ajali mbaya katika eneo la Kabati kwenye barabara A�kuu ya Thika- Murang’a . Kinyanjui amekuwa akiuguza majeraha yaliyotokana na ajali hiyo. A�Wakati huo huo mipango ya mazishi ya marehemu Gakuru inaendelea katika viwnago vya serikali ya kitaifa na kaunti ikiongozwa na waziri wa habari Joe Mucheru na gavana mpya wa Nyeri A�Mutahi Kahiga. Marehemu A�Gakuru atazikwa Jumamosi nyumbani kwake katika eneo la A�Kirichu kaunti ya Nyeri

A�