Tisho La Islamic State

Wanamgambo wa kundi la Islamic State waliouawa katika shambulizi la angani lililotekelezwa na Marekani walikuwa tisho kwa maslahi ya Marekani na mataifa ya magharibi kwa mujibu wa makao makuu yaA� Pentagon.

Kambi ya kundi la Islamic State ilishambuliwa katika eneo la Sabratha kilomita sabini magharibi ya mji wa Tripoli. WatuA� 38 walioripotiwa kuawa ni pamoja na raia mmoja wa Tunisia kwa jina Noureddine Chouchane ambaye anahusishwa na mashambulizi yaliyotekelezwa nchiniA� Tunisia mwaka uliopita likiwemo shambulizi moja ambapo raia 30 wa Uingereza waliuawa.

Kundi la Islamic state limekuwa likitekeleza shughuli zake nchini Libya kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Libya ingaliA� inakabiliwa na ghasia miaka nne baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Muammar Gaddafi.

Juhudi zaA� kubuni serikali ya muungano zimeshindwa kuzaa matunda huku makundi mbalimbali yakitawala maeneo mbalimbali nchini humo.