Timu ya taifa ya Raga yaanza kampeni yake ya raundi ya tano ya msimu huu wa msururu wa HSBC

Timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande, itaanza kampeni yake ya raundi ya tano ya msimu huu wa msururu wa HSBC dhidi ya Ufaransa Jumamosi hii, nchini Marekani.A� Baada ya kujinyakulia alama 13 katika raundi ya nne jijini Hamilton, New Zealand, alama za juu zaidi msimu huu, Shujaa sasa itaangazia kuboresha matokeo hayo nchini Marekani na Kanada. Timu hiyo inayofunzwa na Innocent Simiyu, itachuana na Ufaransa katika mechi yake ya ufunguzi, kisha icheze na Urusi na hatimaye kukamilisha michuano yake ya kundi dhidi ya Fiji. Shujaa inashikilia nafasi ya nane jedwalini kwa alama 35 baada ya raundi nne msimu huu. Mabingwa Afrika Kusini wanaongoza kwa alama 77, huku wakifuatwa na New Zeland na Fiji kwa alama 69 na 62, mtawalia.