Timu ya taifa ya ndondi Huenda Isishiriki Michezo Jijini Younde, Kameruni

Timu ya taifa ya ndondi ambayo imekuwa kambini kwa majuma kadhaa ikijiandaa kwa michezo hiyo ya kufuzu itakayoanza tarehe tisa hadi 12 mwezi huu jijini Younde, Kameruni, huenda isishiriki iwapo serikali haitatoa shilingi milioni sita nukta tano zinazohitajika kugharamia safari hiyo.

Wakati uo huo, kikosi hicho kiliendelea na mazoezi yake huku mabondia wakionekana kuwa wenye motisha wa hali ya juu kabla ya kuondoka tarehe sita.

Kocha mkuu Patrick Maina alielezea matumaini ya Kenya ya kujinyakulia nafasi zaidi kuliko jinsi ilivyokuwa katika michezo ya mwaka 2012 .